{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

WATANZANIA NA TABIA YA KULALAMIKA NA KULAUMU, soma hapa kujifunza mengi na kuacha tabia ya kulaumu na kulalamika


Mbona unalalamika kila siku kwamba biashara yako ni ngumu? Kwani wewe ulianzisha biashara yako kwa lengo gani? Malalamiko kutoka kwa wajasiriamali imekuwa ni sehemu ya Maisha yao. Kila unapojaribu kuongea na wajasiriamali lazima usikie malalamiko mengi ikiwemo--
ukosefu wa mitaji ya kuendesha biashara.
Watu wanalalamika eti hawafikiriwi, hakuna anayewajali na hawasaidiwi! Yawezekana ni kweli, lakini kwa yeyote mwenye malalamiko na aketi chini na ajiulize hili; “Ndiyo hakuna anayenijali, hakuna anayenifikiria na hakuna anayenisaidia, kwahiyo…...”
Ukishajiuliza swali la “kwahiyo…” --bilashaka utaamua mojawapo kati ya haya:
ama ni kuacha kufanya biashara au kuendelea na biashara”. Endapo utaamua kuacha biashara kero na malalamiko yako yote vitakuwa vimeishia hapo na kimsingi utaweza kuendelea na maisha mengine.
Endapo utachagua kuendelea na biashara, maana yake ni kwamba matatizo unayolalamikia si makubwa kiasi cha kukuzuia kupata faida na pengine ndiyo maana umechagua kuendelea na biashara bila kujali matatizo na changamoto zilizopo.
Utamaduni wa kulalamika juu ya kazi tunazozifanya tumeurithi kutoka kwa watumishi hasa waajiriwa. Mfumo wa ajira duniani uko katika umbo la pembe tatu (piramidi). Ambapo unakuta mkubwa ni mmoja na chini yake kunakuwa na watu wengi kutegemea na ukubwa wa taasisi au kampuni husika iliyokuajiri. Mara nyingi watu walioko chini wakishindwa jambo lolote umsukumia yule aliyejuu ili afikiri na kutoa suruhisho kwaniaba ya wale wote anaowaongoza.
Kwa maana nyingine ni kwamba katika umbo hilo hapa juu, kuna mambo mengine huruhusiwi kuyafanya au kuyatolea maamuzi isipokuwa aliye juu yako. Pili, ukiwa mwajiriwa wa ngazi za chini kuna mambo ambayo yakikushinda unayapeleka kwa mkubwa wako kwaajili ya ufumbuzi zaidi.
Kwahiyo, chimbuko la tabia ya kulalamika ni utaratibu wa kutegemea maamuzi ya aliye juu yako. Kama anayepaswa kuamua jambo fulani, hafanyi hivyo kwa wakati au akafanya maamuzi vibaya basi utakuta waajiriwa walioko chini wanafanyakazi kwa kunung’unika muda wote, wanalalamika muda wote wanasema hovyo muda wote na hasa wakiwa maeneo ya nje ya ofisi zao.
Ikumbukwe kuwa, kinachowapa waajiriwa uhalali wa kulalamika ni ule mfumo au utaratibu wa ajira duniani ambao unatoa nafasi kwa mwajiriwa kuweza kupeleka malalamiko yake ngazi za juu endapo ataona kuna mambo ambayo hayaendi sawa.
Katika mfumo mzima wa ajira “MKUU” ni mtu wa mwisho na hatutarajii halalamike kwasababu hakuna mtu mwingine aliye juu yake ambaye anatakiwa kumpelekea malalamiko, ingawaje wengine ujikuta nao wakilalamika kwa watu wa chini yao. Wewe kama ni “Mkuu” kazi yako ni kuamua na kutenda basi!

*@Mr motivation*
Share:

MAMBO MAZURI MUDA MWINGINE HUPITISHWA KWENYE NJIA MBAYA,soma hapa kujifunza mengi na update hamasa


Hivi umewahi kumuona mdudu kiwavi, kiwavi
ni mdudu mwenye sura mbaya sana na
mwenye umbo baya sana, kwasababu
anapokuwa kwenye harakati za ukuaji
anakuwa kama mfano wa jongoo, lakini kitu
kimoja ambacho kinanishangaza kutoka
kwenye huyu mdudu ni kwamba ni yeye huyu
huyu ambae siku moja anakuja kuwa kipepeo,
najiuliza tu swali moja unadhani kwa kipindi
hajawa kipepeo angesema basi bora nife kama
ndo niko hivi,kipepeo angetokea?laa hasha
asingetokea, angesema mimi ndo nimeumbwa
hivi hivi na maisha yangu ndo haya haya
Mungu kanionea namatumaini leo
tusingeuona uzuri wa kipepeo.
Na maisha yetu ndivyo nalivyo muda
mwingine mambo mazuri huwa yanapita
kwenye matukio mabaya ambayo huenda
huyapendi, siku moja alikuepo jamaa mmoja
alikuwa amechoka kabisa kufanya kazi
ambayo anaifanya, huenda ni kama wewe
ulivyochoka kwenda kazini kwasababu
unaamka mapema sana, huyu bwana kila siku
akawa anamuomba Mungu apate kazi kubwa ,
nzuri na yenye mshahra zaidi ya ule ambao
alio nao kwasasa.lakini apate kazi
ambayoatakuwa na furaha, aliomba saana tu,
siku moja Mungu akajibu dua yake, alipewa
kazi na boss akachelewa kuiwasilisha
kampuni ikakosa tenda, basi kesho yake
alipofika kazini alikuta barua ya kufukuzwa
kazi.
Daaah jamaa alilia sana sana tu kwanini
amefukuzwa kazi, familia yake itaishije,
siunajua wafanyakazi huwa wakiwa kazini
wanakuwa wameridhika eee hawawazi hata
kufanyabiashara au mambo yanaweza
kuwaingizia kipato cha ziada kwa muda wa
ziada, basi alilia sana nakuanza kumlalamikia
Mungu kuwa amemuomba apate kazi sasa
ndo kafukuzwa kabisa.
Baada ya kuteseka kwa muda kidogo na
maisha kuwa magumu kwaajili ya kufukuzwa
kazi akapata muda wa kuwa anasoma
magazeti kupoteza mawazo, siku moja
akakuta gazeti kuna kampuni imeanzishwa
anatakiwa mfanyakazi mwenye sifa kama
zake, akaenda kufanya usaili akafanikiwa
kupata kazi, akapata cheo kama kile kile
alichoomba kwa Mungu, mshahara ule ule na
akawa free, sasa tujifunze kitu unadhani
aisingefukuzwa kazi angepata muda wa kukaa
kusoma gazeti na kupata habari iyo kiukweli
ingekuwa ngumu.
Rafiki usihuzunike unapokuwa kwenye wakati
mgumu, kwenye wakati ambao Mambo
hayaendi sawa, jua Mungu anakutafutia nafasi
iliyobora zaidi endelea kupambana hadi
kileweke, dhahabu ili ing'ae sharti ichomwe
moto, usikate tamaa usihuzunike siku moja
utakuja kuishi maisha yaliyo bora.
USIHUZUNIKE MDUDU KIWAVI, SIKU MOJA
UTAKUWA KIPEPEO
Asante kwa kutembelea na Endelea kutembele blog yako ya Maki inspire kwa elimu said I.
*@Mr motivation*
Share:

JE, NINI CHA KUFANYA USIPOONA MATUNDA YA KAZI UIFANYAYO


Unakumbuka wakati unaanza kazi, kuna vitu
ambavyo ulitamani sana kuwa navyo,
ulitamani kuwa na chumba chako, angalau
chumba na sebule, kitanda, TV, kajiko ka gesi,
na vikorokocho vya ndani. Hembu angalia vile
vitu kama unavyo au huna na ulivipataje,
jiulize baada ya kuvipata pesa ya mshahara
uliyotumia kununua vile vitu iko wapi kama
sasa hivi huvinunui tena? Unajua ni kwanini
ulivipata hivyo vitu?
Huna haja ya kuumiza kichwa sana, ulivipata
kwakuwa ulikuwa na malengo na mtu
anapokuwa na mlengo flani basi moja kwa
moja huilazimisha akili yake kufanyakazi
kuelekea yale malengo. Kuna namna mbili za
kuweka malengo, namna ya kwanza ni kuweka
malengo bila kujijua “Unconscious Goals” aina
ya pili ni kuweka malengo ukiwa unajijua
“Conscious Goals”.
Aina hii ya kwanza ni ile ambayo kuna vitu
unapanga kuvifanya lakini si kwa mpangilio
au hukai chini ukasema haya ni malengo
yangu. Kama ambavyo ulisema unatamani
kununu TV na ukanunua hayo ni malengo
ambayo ulijiwekea, aina ya pili ni ile ambayo
unakaa chini na kuandika au kusema kabisa
mwaka huu nataka kufanya kitu A, B, Cna D.
Katika maisha mafanikio au vitu havidondoki
tu kama mvua ni lazima uviwaze na
kuviwekea malengo iwe ni kwa kujua kuwa
haya ni malengo au si malengo. Kwa watu
wengi ambao hawafanikiwa wanajikuta kuwa
badala ya kuweka malengo basi huweka
vikwazo. Kwamba kwa kuangalia mshahara
wako badala na kuuona mdogo badala ya
kuweka melango kutokana na mshahara wako
mdogo basi unajiweka vikwazo kutokana na
mshahara wako mdogo.
Hembu nifafanue kidogo, tuchukulia unapata
mshahara wa shilingi laki mbili kwa mwezi na
akiba ni shilingi elfu hamsini, kwa maana
kuwa hata ukijibana vipi utabakia na shilingi
elfu hamsini. Sasa umepata kiwanja cha
shilingi milioni moja, watu ambao
hawafanikiwi watawaza hivi “Mshahara wangu
mdogo siwezi kununua kiwanja cha milioni
moja”.
Lakini watu waliofanikiwa huweza hivi “Milioni
moja nikikusanya elfu hamsini hamsini, kwa
mwaka nitakuwa nalaki sita, hizi laki nne
zilizobaki kununua kiwanja ...ngoja niangalie
ofisini…siwezi pata mtu wa kunikopesha
kweli…hapa nikipunguza kupanda Bajaji…vipi
nikiwa napika mwenyewe si nita save…na
nikiuza na ile deki ya CD ambayo siitumiii…si
zitafika kweli…kuna na lile dili ofisini ngoja
ni….”
Umeona tofauti ya watu hawa wawili, yule
wakwanza baada tu ya kuona kuwa elfu
hamsini haitoshi kununua kiwanja cha milioni
moja alikaa kimya akasahau na
kujisahaulisha tena kuhusu kiwanja. Tena
utamsikia akisema “Sitaki kujipa tamaa za
bure, haya maisha ni lazima uridhike na
unachopata…” Lakini wapili yeye ataumiza
kichwa mpaka kupata anachokitaka, hivyo
ndivyo unavyotakiwa usiangalie usicho nacho
bali namna ya kupata cha kuongezea.

Asante kwa kutembelea blog yako ya makinspire.blogspot.com. karibu tena kwa kujifunza mengi zaidi
*@Mr motivation*
Share:

FAIDA ZA KUJITAMBUA,soma hapa kujua faida kuu zitokanazo na kujitambua



Kuna faida nyingi sana zinazotokana nakujitambua, chache kati yake ni hizi :
1. Kuishi maisha yaliyo kamiliKujitambua kunakupa nafasi yakupanga malengo kutokana na ndotozako maishani. Malengo ndio msingiwa maendeleo. Tatizo ni kuwa wengiwetu tumejawa na hofu, kutojiamini,kuiga, kutojua cha kufanya nakutofahamu umuhimu wa fikra zetukwenye maisha ya kilasiku. Kujitambua kunakupa ujasiriwa kupambana na vikwazo katikasafari ya kutimiza ndoto zako.Kwa ufupi, kujitambua ni mwanzo wakuishi maisha yaliyo kamili, kifikrana kimtazamo . Unaweza kufanyamambo mengi bila kujitambua, lakinimafanikio yanayodumu hayaji kwakubahatisha, bali kwa kuelewa njiamadhubuti za kufanya mambo iliuweze kufikia malengo. Hiiinawezekana kwa kuanzakujitambua.

2. Kutumia kila fursa ipasavyoFursa ziko kila sehemu, unachohitajini malengo madhubuti unayotakakutimiza. Una utashi mkubwana vipaji vingi vinavyoweza kutumikakatika kutumia fursa mbalimbali nakuinua maisha yako. Njia pekee yakuanza kufahamu uwezo wakomkubwa ni kujitambua.Kujitambua ni kufahamu fursaunazotaka kuzitumia kuendelezamaisha kwa kufanya yale muhimuna kuacha yasiyo na tija kwako.

3. Kujiendeleza zaidi kifikraFikra zako zina mchango mkubwasana katika kuendesha maisha yako.Ili kubadili maisha, ni lazimakubadili fikra. Kubadili fikra ni kitucha kwanza na cha msingi.Ili tuweze kufikia malengo,tunatakiwa kupanua wigo wa fikrazetu na kuona mbali zaidi ya leo nakesho. Hii inawezekana kwa kilammoja wetu, ingawa si kazi rahisi.

4. Kuwa mchango mkubwa kwajamiiBinafsi naamini – maisha huwa namaana zaidi kama kile unachofanyakitakuwa na mchango mkubwa kwawatu wengi zaidi .Mtu anayejitambua huwa rasilimalimuhimu kwa jamii. Mchango wakehuwa chachu ya mabadiliko katikamaisha ya wengi. Maendeleo huletwana watu wenye mtazamo chanyazaidi juu ya malengo yao maishani.Nawe pia unaweza kama ukianzakujitambua.Kujitambua ni jambo muhimu sana ilikuweza kufanikiwa kwenye maisha yako.Ni chaguo lako – kuchukua nafasi nakuweza kujitambua au kuishi maishauliyozea na kuendelea kushabikia walewanaotimiza ndoto zao kila siku.Karibu kwenye safari ya kujitambua.
Share:

HUKU NDIKO KUTAJIRIKA KWA KUPATA PESA NYINGI

Kupata pesa nyingi kunahitaji
ubunifu wa hali ya juu hasa katika masuala
ya uwekezaji. Ubunifu si kitu cha kutazamia
bali ni kitu ambacho lazima ufikiri kwanza
ndipo ukipate. Hali halisi ya maisha ni
kwamba, watu wengi hawapendi michakato
ya pesa inayowasumbua akiri zao. Matokeo
yake wanaishia kufanya michakato kama ile
inayofanywa na wengine wengi. Matokeo yake
nao wanapata pesa kama wenzao au pungufu
ya wenzao.
Unapofikia hatua ya kupokea pesa kama pesa
unakuwa umepokea “kazi iliyoisha” . Kwa
maana hiyo, uhitajiki tena kufuata mchakato
wa kusubili, kuvumilia, kulipa gaharama
kabla n.k, kama mwanzo. Ukiona watu
wanashangilia wanapopata pesa hasa
ambayo hawajaifanyia kazi, basi ujue kuwa
wanajisikia amani sana kwasababu,
wanakuwa wameepukana na kazi kama vile
kutenga muda, kulipa gharama kabla,
ubunifu, kuvumilia, kusubili n.k.
Kwakuwa pesa ni matokeo ya mchakato, ni
wazi kwamba kila mchakato una mwenyewe
na kwa maana hiyo, kila pesa ambayo haiko
mfukoni mwako ina mwenyewe. Kama wewe
ni mtu wa kufuata njia za mkato kila mara, ili
kupata pesa basi ujue kuwa kutajirika kwako
ni muujiza. Kwasababu, wale wote wenye
pesa zao watakuwa kama ukibahatika
wanakupa pesa kidogo sana na kwa muda
ambao wanajisikia kufanya hivyo bila kujali
shida zote ulizonazo.
Kwa upande mwingine, pesa unayopata kwa
kukwepa mchakato wa upatikanaji wake, ni
vigumu sana kubaki nayo, kwasababu pindi
unapoitumia ikaisha, huwezi tena kupata
pesa nyingine mara moja. Hii ni kutokana na
ukweli kwamba wewe unayepata pesa nje ya
mchakato wake unakuwa huna umiliki
wowote wa mchakato huo.
Unapoanzisha na kumiliki mchakato wa
kuzalisha pesa ni kwamba ikitumika ikaisha,
basi mchakato wako unaoumiliki unazaa tena
pesa nyingine. Kwahiyo, unaendelea kuvuna
pesa nyingi bila kikomo – Huku ndiko
kutajirika!
Tunahitaji kutambua kuwa matajiri wengi
duniani walianzisha na kusimamia michakato
ya kuleta pesa. Ndiyo maana wengine
pamoja na kwamba walishafariki, bado ile
michakato waliyoianzisha na kuijenga mpaka
leo inaendelea kutoa pesa.
Sasa imefika zamu yako kuanzisha na
kujenga michakato ya kudumu ya pesa. Na
huu ndio wakati muhafaka wa kujitoa kwenye
kundi la wapenda “pesa au mikate” ya bure.
Jijengee tabia kama ya matajiri ambao
upendelea zaidi michakato ya kuleta pesa
kuliko pesa yenyewe.

Share:

MAPATO YASIYO NA KIKOMO,soma hapa kujua nini maana ya mapato yasiyo na kikomo

Unapoongelea suala zima la mapato yasiyo
na kikomo ni sawa na wewe kufunga bomba la
maji mtoni, ili kuleta maji nyumbani kwako.
Maji yakishafika nyumbani wewe unayatumia
unavyotaka na hayakatiki. Wale wote
wasiofikiwa na mabomba ya maji majumbani
mwao, wao wanachokifanya ni kuchota maji
kwa kutumia vifaa kama ndoo, madumu n.k.
Watu hawa wakishapata maji, wanayatumia
na inafika wakati yanaisha. Mara tu maji
yanapoisha, inawabidi wafunge safari tena
kwenda kuchota maji popote yalipo, na
mzunguko unakuwa hivyo maisha yao yote.
Ukichota maji yanakuwepo nyumbani,
usipochota maji hayapo LAKINI yule mwenye
bomba anaendelea kupata maji masaa yote,
hata akiwa amesafiri maji yapo tu!.
Mfano huu wa maji ni sawa na mfumo wa
mapato tunayoyapata. Kwa maana nyingine ni
kwamba, wale wote tunaopata mapato hai au
mapato ya ajira (mshahara), tunafanana
kabisa na wale watu wanaochota maji mtoni
kila siku kwa kutumia ndoo, madumu n.k. Kwa
mfano: Mapato ya ajira -unalipwa siku
unapofanya kazi, usipofanya kazi haulipwi,
ukisafiri bila ruhusa haulipwi, ukiugua muda
mrefu hulipwi n.k.
Kwahiyo, mapato bila kikomo ni mapato
anayopata mtu pasipo kuwa na ulazima wa
kushughulika au kufanya kazi kwa wakati huo.
Mapato haya mara nyingi yanatokana na kazi
au shughuli uliyokwisha kufanyika kitambo na
kuendelea kupata mapato hayo “kimya kimya”,
kutokana na ukweli kwamba watu wengine
wanakuona tu umekaa lakini kumbe wewe
unaingiza pesa nyingi mfukoni.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba mapato au
pesa isiyo na kikomo ni ile ambayo mtu
huipata mara kwa mara, lakini kwa kutumia
nguvu kidogo sana katika kuiendeleza. Mfano;
ni pesa itokanayo na haki miliki kama;k.m.
pesa ya mrahaba au “royalties” kutokana na
kuuza vitabu, album au kukodisha hakimiliki;
faida benki; kodi ya majengo au mashine; au
pesa kutoka kwenye biashara ambayo
haikuhitaji tena wewe kuwepo moja kwa moja
kama “biashara ya kupashana habari au
mtandao”. Hii ni mifano tu ya vyanzo vya pesa
isiyo na kikomo. Aina hii ya mapato
inapatikana baada yaw ewe kufanyakazi kwa
bidii sana kwa muda fulani (k.m. miaka 2
hadi 5), baadae unaendelea kupata pesa kwa
muda mrefu bila hata wewe mwenyewe
kushughulika tena au zaidi.
Uzuri wa mapato yasiyo na kikomo ni
kwamba, unaendelea kupata pesa kwa muda
mrefu baada ya kazi ya uzalishaji au ya awali
kukamilika. Hali hii ya wewe kupata pesa bila
kulazimika kufanya kazi tena ndiyo
ukuwezesha wewe kupata MUDA wa ziada na
hivyo kupata fursa ya kuwekeza muda huo
kwenye mambo mengine. Uzuri mwingine wa
mapato haya ni kwamba duniani kote
hayatozwi kodi kubwa kama mapato ya aina
nyingine
Share:

NYAKATI NGUMU ZA MAISHA, kama kunawakati unapitia kwenye wakati mgumu sikiliza ujumbe huu



makinspire.blogspot.com
Share:

USHAURI WANGU KWAKO


(1)Kamwe usidharau kidogo ulichonacho kwani
kitaweza kukuzalishia kikubwa.
(2)Mpenzi wako akikuacha wakati umepatwa
na shida mwambie "umeniacha kwa shida
zangu maana hujui nilikotoka na pia
nakushukuru kwa kua umenipa nafasi ya kuja
kufurahia raha zangu mwenyewe baadae".
(3) Mtu akikuzarau kwa kua huna kitu basi
mshukuru na upambane kwa bidii ili aone
wivu wa kukusifia na kukusogelea pale
unapozipata au unapofanikiwa.
(4)Mwogope mtu ambae hakutii moyo pale
unapoanguka ila anakua wa kwanza
kukupongeza unapoinuka kwani neno moja la
kutia moyo lina nguvu zaidi ya maneno mia
ya pongezi
(5)Kumbuka ulikotoka ni mbali zaidi ya
unapokwenda hivyo usikate tamaa mafanikio
yapo karibu..
Share:

UMUHIMU WA KUWA NA MAALIFA KICHWANI KWAKO,jua umuhimu wa maalifa maishani kwako


Kila maarifa yaliyopo kichwani ya kazi yake.
tumekuwa tukienda kuomba kazi na kufanya
usaili kwenye maofisi ya watu mbali mbali ili
mradi tupate ajira. Unapokwenda kwenye
usaili mara nyingi hauingii na hata karatasi,
lengo kubwa linakuwa ni kujua una uwezo na
maarifa kiasi gani kuhusu ulichokisoma na
kama unaweza kuleta tija kwenye kampuni
husika? Baada ya kufanya usaili wanaweza
kukuajiri na kukupangia kiasi fulani cha
malipo ambacho ndicho kinakuwa sawasawa
na thamani ya maarifa yako. Ndio maana
kuna viwango vya mishahara kazini. Ofisi
Nyingi mtu anapoenda kusoma akirudi
mshahara huongezeka, ni kwa sababu
ameongeza kiwango cha maarifa kichwani
mwake. Unapongeza maarifa mbalimbali
kichwani mwako na ya maisha ya kawaida ya
watu wengine ndivyo thamani yako Hupanda
kwa maana nyingine... Mshahara unaolipwa
na maarifa yako vinatosha na vinaendana
kabisa.
Tumekuwa kizazi kisichoweza kuhoji na
kuthibiti ujinga unaofanyika, kizazi
kisichoweza kijisimamia maamuzi. Kimekuwa
kizazi cha ndiyo kama yule alivyosema, ni
kizazi cha bendera fuata upepo. Ukisoma
biblia Wagaratia 3 mstari wa kwanza utaona
maandiko yanayoanza na kushangazwa kwa
kizazi kutokuwa na akili na nani alikiloga?
Familia nyingi zilizo bora kwenye maisha yetu
ya kila siku ni familia ambazo ziliwekeza
kwenye maarifa siku za nyuma kwenye maisha
yao ya kila siku. Mara nyingi tumepiga kelele
kuhusu swala la maendeleo na vitu
mbalimbali lakini tunashindwa kujiuliza je
watu walitumia muda gani kuwekeza katika
maarifa. Wahenga walisema, "Alivyo baba na
mama ndivyo watoto walivyo". Tumeendelea
kupiga kelele kwamba Tanzania kuna anguko
la elimu (maarifa), maana yake tumejua kuna
athari zake katika vizazi vijavyo. Unapokuwa
na maarifa zaidi ni rahisi kuwasaidia hata
watoto wako kwenye njia iliyo bora.
Usiwalaumu watoto wa kizazi hiki bila kujua
uwezo wa wazazi wao katika kuwekeza kwenye
suala zima la maarifa. Je wanatumia muda
gani na wanawekeza kiasi gani. Narudi
palepale. Maarifa ni jambo la urithi kwa
watoto kama ulivyo ujinga. Kama hautaki
watoto wako wawe wajinga siku zote wekeza
kwenye maarifa, nao watafaidi katika maisha
yao yajayo hata usipokuwepo.
Share:

KAMA SI LEO KESHO YATATIMIA USIKATE TAMAA

KAMA SI LEO, KESHO YATATIMIA
Jana usiku nikiwa najisomea nilikutana na
msemo huu (If you want to hide something
from a black man, put it in a book), ambao
ulinitia hasira kidogo na kunifanya nijiulize
mara mbili mbili kwanini. Msemo huu miaka
ya nyuma ulitumika nchini Marekani ambapo
ulikuwa una lengo la kuwabagua watu weusi
kupata haki ya msingi ya kujifunza maana
walikatazwa kusoma na kujifunza vitu kadha
wa kadha. Lakini baada ya kufuatilia kidogo
nilikuja kugundua tatizo halikuwa kwa
waliotunga aina hii ya taratibu bali lilikuwa
kwa waliowekewa utaratibu huu. Watu weusi
walikuwa ni watu wasiopenda kujifunza na
kusoma, badala yake waliamua kutumia muda
mwingi kufanya vitu visivyo na tija kwa muda
mrefu ambavyo vilitumia nguvu zaidi kuliko
akili zaidi.
Ndugu zangu mnaosoma makala yangu
niwakumbushe kuwa kizazi cha leo kinajua na
kufahamu mengi lakini hakipendi ukweli. Ni
kizazi kinachosahau mapema na kupoteza
kumbukumbu, ni kizazi cha vita ya kweli na
uhuru, ni kizazi kilichogeuka utumwa wa mwili
na akili, ni kizazi kilichopoteza uhalisia kama
enzi za wazee wetu na viongozi wetu. Ni
kizazi hiki cha hasira, ni kizazi ambacho watu
wanapretend kufurahia au angalau kutoa
meno nje lakini wamejaa shida tupu mfukoni
na kichwani hakuna kitu kabisa.
Share:

USUKATE TAMAA, PAMBANA

 Nilisoma historia
ya mwanasayansi mmoja Thomas Edson
ambaye ndiye aliyegundua taa/bulb za umeme
ikanitia moyo sana. Huyu bwana alifanya
majaribio 10,000 ili aweze kugundua taa
tunazozitumia leo na yote yakafeli. Watu
wakamwambia sasa ni vizuri ukaachana na
hilo jaribio maana umefeli vya kutosha. Huyu
bwana akasema sijafeli ila nimejifunza mara
10,000 jinsi ambavyo fomula zangu hazifanyi
kazi na naedelea kuboresha. Mwishoni
akafanikiwa kugundua taa na kuanzisha
kampuni kubwa sana duniani ya umeme
inayoitwa General Electric Company ambayo
ipo na inazidi kukua hadi leo. Historia ya
huyu bwana inafanana na ya Ford, Honda,
Rais Linkolin wa Marekani na wagunduzi wa
ndege. Hata katika mazingira ya
wafanyabiashara na wafanyakazi wetu
nimekutana na watu waliofilisika, waliopata
hasara, waliofukuzwa kazi, waliofeli shule,
walioshindwa katika mahusiano na
waliokatishwa tamaa sana. Lakini napenda
kuwatia moyo kwa kuzingatia elimu
tunayopata kwa watu waliofanikiwa kuwa;
i) Usikate tamaa, kufeli ndiyo kujifunza mbinu
mpya
ii) Kufeli na kupata hasara ni gharama/ada ya
mafanikio utakayopata baadaye
iii) Kufeli ni nafasi mpya ya kuanza tena,
lakini ukiwa umejipanga vizuri zaidi
iv) Changamoto yeyote usipokuua
inakuimarisha zaidi
v) Usirudi nyuma hata kama changamoto ni
kubwa
vi) Ukiamini unaweza, unaweza na ukiamini
huwezi, huwezi
vii) Kufeli kunakupa shule ambayo hutasahau
daima.
Asanten sana, kwa wote unaosapoti na
kunifanya niendeelee kufanya kazi hii ya
kuelimisha uma wa watanzania kwa ujumla,
shukrani sana,
NakaribishA maoni maoni na ushauri karibun
sana.
Share:

WEKA MAKENGO


Anza kuwa na malengo, ili akili yako ifanye
kazi vizuri nilazima ijue inafanya kazi kwaajili
gani? Nilazima uiwekee malengo nah ii
itakusaidia sana kuona fursa
zinazokuzunguka. Kama ambavyo huwezi
kwenda chooni bila kubanwa na haja ndivyo
hivyo hivyo huwezi kununua kiwanja au
kufungua biashara kama huna mpoango wa
namna hiyo.
Mipango ndiyo huleta ulazima wa kufanya
baadhi ya mambo. Amua ni kitu gani unataka
kukifanya, kwa mfano unaweza kusema kuwa
mwaka huu nataka kufungua biashara ya kitu
flani, ukishakuwa na wazo hilo tu akili yako
itaanza kuwaza ni vitu gani vinahitajika ili
kuifungua hiyo biashara na vinapatikanaje,
hapo moja kwa moja utakuwa umeijaza akili
yako na mambo chanya.
Lakini bila kuwa na malengo akili yako
inakuwa haifanyi chochote, ipo tu na
haisjishughulishi. Hutaona fursa mpya,
kwanza hutakuwa na haja ya kuzitafuta
kwakuwa huzihitaji, utajikuta matumizi yako
yapo kwenye mambo yasiyo na msingi
kwakuwa huna malengo. Lakini kama una
malengo ya maendeleo sidhani kama utafanya
mambo ya kipuuzi, huwezi kununua
smartphone ya laki tatu wakati una lengo la
kununua kiwanja cha laki tano.
Akili yako yenyewe bila kuiambia itafanya
maamuzi ya kupima kipi cha muhimu kati ya
smartphone ya pili au kiwanja cha kwanza.
Anzia hapo kwa kuwa na malengo, kisha weka
mikakati ya kuyafikia hayo malengo na
utajikuta ni mtu mpya, utaona namna
ambavyo kiasi kidogo unachopata sasa
unaweza kukiwekeza kwa faida na kuacha
kuwa mtu wa kulalamika, watu wote
waliofanikiwa walishaweka mapengo ya
kufanikiwa weka yako sasa.
Akili zetu zimetengenezwa kwa namna
ambayo zinafanyakazi kutokana na malengo
flani. Hii ndiyo maana katika kipindi ha
mitihani wanafunzi huhangaika kusoma sana
kwakuwa kuna mitihani, kusingekuwa na
mitihani akili isingehangaika namna hiyo
kutafuta mbinu za kufaulu. Weka mlaengo ya
kufungua biashara, malengo ya kununua
kiwanja na kufanya uwekezaji wa aina yoyote
ile.
Ukishakuwa na malengo akili yako itaanza
kufanya kazi kuyafikia na utaona namna fursa
zitakavyoonekana, utaona namna
utakavyopunguza matumizi yasiyo na msingi,
utaona namna ambavyo kila shilingi
utakayoipata utaipeleka kwenye mambo ya
maana na kubwa kabisa utaona mabadiliko
katika maisha yako. WEKA MALENGO.

Share:

MJUE KIJANA ALIYEANZA KUMILIKI KAMPUNI AKIWA NA MIAKA 16,msome hapa kumjua

Kuna kijana anaitwa odense miaka 22
kutoka nchini Uganda anaeitwa Andrew
Mapuya.
Andrew anatokea katika famili ya chini sana
ambapo mwaka 2008 wazazi wake woote
walisimamishwa kazi.Jambo ambalo
lilipelekea nyumbani maisha kuwa
magumu.Wakati huo akiwa na miaka 16 na ni
mwanafunzi wa sekondari ikawa inamlazimu
aokote chupa za plastic auze na anunue
chakula cha nyumbani kwao.
Mwaka huo huo serikali ya Uganda ilipiga
marufuku matumizi ya mifuko ya plastic kwa
sababu za kimazingira pamoja na kiafya.Bila
kupoteza muda Andrew akatambua fursa kuwa
iwapo hakutauzwa mifuko ya plastic bado
mifuko itahitajika je mbadala wake ni nini?
Akawaza aanzishe biashara ya kutengeneza
mifuko ya karatasi yaani paper bag.Akafanya
ufatiti wa uhitaji wake wa mtaji ikawa ni tsh
za
uganda 36,000.Basi akaanza mdogo mdogo
kukusanya chupa za plastic anauza hela
anatunza ili kupata mtaji.Akatunza pesa
mpaka
alipobakiwa na kiasi kidogo kama tsh 11,000
akaenda kumuomba mwalimu shule
akampatia.Mwaka huo huo akasajili kampuni
yake ambayo inasemekana ndio kampuni ya
kwanza kusajiliwa ya kutengeneza na kuuza
mifuko ya karatasi.Kampuni inaitwa Youth
Enterprenual Link Investment (YELI)
Kampuni hiyo sasa inawateja wengi na
inatengeneza na kusambaza mifuko kwenye
super markets,restaurant,medical
centre,maduka,na makampuni mbali mbali
katika mji wa Kampala.Mpaka sasa
ameshaajiri
vijana zaidi ya 16.
Mwaka 2012 alikuwa mshindi wa shindano la
Anzisha Prize la vijana wajasiriamali na
alishinda dola za kimarekani 30,000
Ninachoweza kuona kama funzo kutoka kwa
kijana huyu ni kuwa
1.Unapotaka kuanzisha biashara fanya utafiti
2.Fanya biashara kwa kuangalia uhitaji wa
bidhaa husika yaani jamii inapungukiwa kitu
hicho
3.Kunapokuwa na shida ya kitu flani sehemu
flani hiyo ni Fursa ina maana unatakiwa
kuanzisha baiashara ili utoe suluhisho,ili utoe
huduma na automatical ndio biashara sasa
maana ina wateja.
4.Kwa vijana usisubiri mpaka uwe mtu mzima
ndio uanzishe biashara.Anzakuwaza mafanikio
sasa,anza kupanua mawazo yako na uchukue
hatua
Share:

BADILI UNAVYOWAZA KAMA UNATAKA FANIKIWA


Kama untaka kufanikiwa ni lazima ubadili
namna unavyowaza. Acha kuangalia
mshahara au kipato chako kidogo kama
kikwazo bali kama fursa. Usiangalie nalipwa
kidogo hivyo siwezi hili na lile bali angalia
kuwa nalipwa kaisi flani hiki kinaweza kuwa
kianzio cha kufanya moja, mbili, tatu. Hakuna
mshahara mdogo wala mkubwa bali kuna
matumizi mdaogo na makubwa, namna
unavyotumia kile unachokipata ndiyo itaamua
kile unachokiwekeza.
Kuna watu wanalipwa milioni tano kwa mwezi
lakini ikifika Tarehe 20 bado hawana hata
shilingi kumi na kamwe mishahara
haigongani, lakini kuna wtau wanalipwa laki
mbili lakini mishahara hugongana benki.
Badili fikra kuhusu kile unachokipata na
kukiona kama kianzio cha kufanya lolote.
Hata kama kinaweza kununua matufali mawili
tu jua kuwa ni mwanzo mzuri wa kujenga
nyumba, badili namna unavyowaza.makinspire.blogspot.com



Share:

Usikate tamaa mwanaliaza dada Heather Dorniden alianguka chini akainuka akashinda na kuwa wakwanza



makinspire.blogspot.com
Share:

NINI CHA KUFANYA USIPOONA MATUNDA YA KAZI UIFANYAYO

Unakumbuka wakati unaanza kazi, kuna vitu
ambavyo ulitamani sana kuwa navyo,
ulitamani kuwa na chumba chako, angalau
chumba na sebule, kitanda, TV, kajiko ka gesi,
na vikorokocho vya ndani. Hembu angalia vile
vitu kama unavyo au huna na ulivipataje,
jiulize baada ya kuvipata pesa ya mshahara
uliyotumia kununua vile vitu iko wapi kama
sasa hivi huvinunui tena? Unajua ni kwanini
ulivipata hivyo vitu?
Huna haja ya kuumiza kichwa sana, ulivipata
kwakuwa ulikuwa na malengo na mtu
anapokuwa na mlengo flani basi moja kwa
moja huilazimisha akili yake kufanyakazi
kuelekea yale malengo. Kuna namna mbili za
kuweka malengo, namna ya kwanza ni kuweka
malengo bila kujijua “Unconscious Goals” aina
ya pili ni kuweka malengo ukiwa unajijua
“Conscious Goals”.
Aina hii ya kwanza ni ile ambayo kuna vitu
unapanga kuvifanya lakini si kwa mpangilio
au hukai chini ukasema haya ni malengo
yangu. Kama ambavyo ulisema unatamani
kununu TV na ukanunua hayo ni malengo
ambayo ulijiwekea, aina ya pili ni ile ambayo
unakaa chini na kuandika au kusema kabisa
mwaka huu nataka kufanya kitu A, B, Cna D.
Katika maisha mafanikio au vitu havidondoki
tu kama mvua ni lazima uviwaze na
kuviwekea malengo iwe ni kwa kujua kuwa
haya ni malengo au si malengo. Kwa watu
wengi ambao hawafanikiwa wanajikuta kuwa
badala ya kuweka malengo basi huweka
vikwazo. Kwamba kwa kuangalia mshahara
wako badala na kuuona mdogo badala ya
kuweka melango kutokana na mshahara wako
mdogo basi unajiweka vikwazo kutokana na
mshahara wako mdogo.
Hembu nifafanue kidogo, tuchukulia unapata
mshahara wa shilingi laki mbili kwa mwezi na
akiba ni shilingi elfu hamsini, kwa maana
kuwa hata ukijibana vipi utabakia na shilingi
elfu hamsini. Sasa umepata kiwanja cha
shilingi milioni moja, watu ambao
hawafanikiwi watawaza hivi “Mshahara wangu
mdogo siwezi kununua kiwanja cha milioni
moja”.
Lakini watu waliofanikiwa huweza hivi “Milioni
moja nikikusanya elfu hamsini hamsini, kwa
mwaka nitakuwa nalaki sita, hizi laki nne
zilizobaki kununua kiwanja ...ngoja niangalie
ofisini…siwezi pata mtu wa kunikopesha
kweli…hapa nikipunguza kupanda Bajaji…vipi
nikiwa napika mwenyewe si nita save…na
nikiuza na ile deki ya CD ambayo siitumiii…si
zitafika kweli…kuna na lile dili ofisini ngoja
ni….”
Umeona tofauti ya watu hawa wawili, yule
wakwanza baada tu ya kuona kuwa elfu
hamsini haitoshi kununua kiwanja cha milioni
moja alikaa kimya akasahau na
kujisahaulisha tena kuhusu kiwanja. Tena
utamsikia akisema “Sitaki kujipa tamaa za
bure, haya maisha ni lazima uridhike na
unachopata…” Lakini wapili yeye ataumiza
kichwa mpaka kupata anachokitaka, hivyo
ndivyo unavyotakiwa usiangalie usicho nacho
bali namna ya kupata cha kuongezea.makinspire.blogspot.com


Share:

UNAFURAIA KAZI YAKO??

JE UNAFURAHA NA KAZI YAKO??
UKIONA PAYSLIP MWISHO WA MWEZI
UNAFURAHI AU UNAKUNJA USO???
Kama majibu ni ndio unafurahia basi hongera
sana na endelea na kama ni hapana basi
jiulize UNAHITAJI KUWA NA FURAHA AU
HUZUNI??????
Kuna watu mwisho wa mwezi ukifika na
mshahara unapotoka hatuna furaha na
tukiangalia payslip tunakunja uso kwani pesa
zote zinapita tu na kwenda kulipia madeni na
baada ya hapo tunaongeza madeni tena hapo
hakuna maendeleo zaidi ya kurudi nyuma
Wangapi at least tunatoka na familia zetu
mara moja kwa mwezi tunaenda SERENA
HOTEL AU BAHARI BEACH AU SEA CLIFF
KUREFRESH MIND AU AT LEAST MARA MOJA
KWA MWAKA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA
KITALII WEWE NA FAMILIA YAKO???
FIKIRI UMEFANYA KAZI MIAKA 10-15 LKN
BADO UNAPANGA AU KUJENGA NYUMBA
MOJA TU AMBAYO SIO UNAYOIPENDA,HUNA
USAFIRI BINAFSI,WATOTO HAWAENDI SHULE
UIPENDAYO VYOTE HIVYO VINAKUPA STRESS
NA MAWAZO UNAONEKANA MZEE WAKATI
BADO KIJANA,UNAPATA MARADHI YA AJABU
UKIWA NA UMRI MDOGO NA MENGINE
HUONEKANA UKIWA MZEE KWANI MUDA
MWINGI HUNAFURAHA NI MAWAZO
TU.Hutamani kustaafu hata kama umri
umefika kwani hakuna ulichowekeza kwa
miaka zaidi ya thelathini uliyofanya kazi na
akaunti zote zipo empty.Mshahara ukichelewa
kidogo pressure juu
KAMA HAUNA FURAHA NA UNGEPENDA
KUWA NA FURAHA BASI BADILI FIKRA ZAKO
ONGEZA NJIA ZINGINE ZA KUKUONGEZEA
KIPATO
Usikae kupoteza muda wako kufanya kitu
kisicho na manufaa kwako au kisichokufurahi
sha maishani mwako kwani hutoweza kufikia
malengo yako
Share:

PESA ZAKO ZINAENDA WAPI

Pesa Zako Zinaenda Wapi?
Hili ni swali ambalo karibu kila mfanyakazi
hujiuliza hasa wale ambao hawanywi pombe
au si watu wa kuhonga, hawana matumizi ya
anasa ya kuonekana. Kwa wafanyakazi wengi
bila kujali matumizi yao yakoje hujikuta
mwisho wa mwezi hawana kitu na husubiria
mishahara kwa hamu. Angalau wale watu wa
anasa wanajua pesa zao zinaenda wapi?
Kabla ya kukuambia pesa zako zinapoenda
kwanza ingekuwa vyema ukafahamu
“Matumizi ya anasa ni nini?”. Kwa watu wengi
matumizi ya anasa ni kununua vitu vya bei
ghali kama vile nguo za gharama, magari,
kunywa pombe, kuhonga sana na vitu kama
hivyo vya kistarehe na hii ndiyo maana watu
ambao hawafanyi hivyo vitu hujiona kama
hawafanyi anasa huku pesa zikiwa
hazionekani.
Lakini hiyo siyo kweli, tafsiri halisi ya
matumizi ya anasa (Kwa mujibu wangu) ni
matumizi yasiyo na msingi wala ulazima
wowote. Kwa maana ya kwamba aina ya
matumizi yote ambayo kama usingeyafanya
yasingeathiri afya yako, heshima yako mbele
ya jamii na huwa hayabadilishi chochote
kama yakifanyika.
Kwa tafsiri hii kuna mambo mengi ambayo
tunayafanya ambayo si ya msingi na hutumia
pesa nyingi bila sisi kujijua, kwa mfano
kununua mashati kumi wakati unavaa
matano, kununua pea 20 za viatu wakati
unavaa tatu tu, kuwa na simu mbili za
smartphone wakati unatumia moja tu kwenye
mtandao, kunywa soda kila baada ya mlo
wakati maji yangetosha, kupanda Bajaji
wakati daladala zipo au ungetembea kwa
miguu ungeimarisha afya yako.
Kuwa na aina tano za pafyum wakati moja
ingetosha, kununua TV ya nchi 40 wakati ya
21 ingetosha, kutoa michango ya haruisi kila
unapopewa kadi, michango ya birthday party,
kushona sare na suti kila harusi, kununua
nguo mpya kila tukio linapotokea wakati
unazo ndani na mambo mengine madogo
madogo ambayo unayafanya mara moja moja
lakini ukikaa chini na kujumlisha unakuta una
mtaji wa duka kubwa la nguo au ungekuwa
ushanunua kiwanja.
Haya mambo hatuyaoni kuwa ni ya anasa
kwakua hatuyafanyi kila siku na kwakuwa
jamii inayaona kama mambo ya kawaida,
lakini kiuhalisia ni mambo ya anasa, tena ya
anasa kuliko hata kunywa pombe. Unaishi
msela au dada mwenyewe una sahani kumi,
vikombe 20 na vitu kama hivyo ambavyo
vimekaa kupamba kabati then what baada ya
kupambika?
Vitu hivi vinaweza kuonekana vitu vya
kawaida, muhimu kuvifanya lakini si kwa mtu
ambaye ndiyo kwanza anaanza ajira, huna
hata kiwanja au sehemu yoyote uliyowekeza.
Katika umri flani na kwa kuangalia kipato
chako, kuna mambo ambayo ili kufanikiwa ni
lazima kuyapunguza au kuachana nayo
kabisa kwani kwa kuyafanya hayakuongezei
chochote na hukupunguzia pesa.
Vitu vyote hivi au aina hii ya matumizi
wazungu huita ‘Liability” Ni vitu ambavyo
havizalishi bali huhitaji kutumia pesa kila
siku. Unapaswa kuwa na “Asset” kwa manaa
ya kitu ambacho kitazalisha au kinapanda
thamani bila kuhitaji kutumia pesa ya
mfukoni. Naamini mpaka hapa umeshajua
pesa zako zinaenda wapi na uko tayari kwa
kujua ni kitu gani cha kufanya?
Share:

ANZA BIASHARA KWA LENGO LA KUTOA HUDUMA BORA SIO PESA

Anza biashara kwa lengo la kutoa huduma
bora na si kwa malengo ya kupata pesa
nyingi. Tofauti ya haya mawili nikuwa kama
lengo lako la msingi ni kutoa huduma bora,
tuseme unafanya biashara ya nyanya na una
malengo ya kuhakikisha kuwa wateja wako
wanapata nyanya nzuri na kwa wakati, kwa
kutimiza malengo yako itawalazimisha wateja
wako kila wanapohitaji nyanya nzuri kuja
kwako.
Hii inamaanisha kwamba wanapokuja kwako
kila mara pesa itaingia. Lakini kama lengo
lako ni kutengeneza pesa nyingi, inamaanisha
kua utafanya kila kitu ili kuingiza pesa na
wakati mwingine utakuwa tayari hata
kuwadanganya wateja wako ili tu wanunue na
wewe kupata pesa. Utapata pesa kweli lakini
wataja hawatarudi tena na utakuwa mwisho
wako.
Lakini si hilo tu, kama unasukumwa katika
kupata pesa ya harakaharaka na pesa
ikakosekana basi ni rahisi kwako kukata
tamaa. Itakukosesha uvumilivu ambao ni kitu
muhimu katika biashara. Badili malengo yako
sasa na wekeza akili yako katika kuboresha
bidhaa zako na huduma unayotoa, pesa
itakuja yenyewe.makinspire.blogspot.com
Share:

FIKIRIA NAMNA YA KUCHUKUA HATUA BILA KUCHELEWA

Hufikiri namna ya KUCHUKUA
HATUA BILA KUCHELEWA .
Watu wanaofanikiwa ni watu
ambao huchukua hatua za
kutekeleza yale waliyojifunza na
wameyaamini.Watu
waliofanikiwa si watu wa
maneno mengi mengi bali ni
watu wa vitendo vingi
vingi,huwa na hali ya uharaka
kwa kila jambo muhimu(sense of
urgency).
Kila siku hujiuliza,leo nifanye
nini bila kuchelewa ili kusogea
hatua moja Zaidi?Hawapendi
kuchelewa kuweka katika vitendo
kila jipya wanalojifunza.
Je nawe unafikiri kwa namna hii
au kuna maeneo unahitaji
kuongeza uwezo wako?
Endelea kutembelea blog yetu ya makinspire.blogspot.com
 Kujifunza
Mafunzo zaiid bila Malipo
Share:

MWANZO NI MGUMU, msome huyu kijana wa kitanzania mwenye umri mdogo alifanikiwa kipesa

VIJANA wengi wamekuwa wakikimbia
kilimo vijijini wakidhani kuwa hakina faida
yoyote.
Hawafahamu kuwa siku zote mwanzo ni
mgumu kwani hata waliofanikiwa awali
walikuwa maskini na hawakuwahi
kufikiria kama watakuja kuwa matajiri
wakubwa duniani.
Kilimo na biashara ni miongoni mwa vitu
vilivyochangia utajiri wa watu wengi ndani
na nje ya nchi. Hata siku moja huwezi
kumiliki mabilioni ya fedha kwa kutegemea
kuajiriwa.
Katika makala haya kutana na
mfanyabiashara wa kwanza wa Kitanzania
kufanya biashara ya kusafirisha korosho
kwenda nchini Vietnam, Abbas Maziku
ambaye anaelezea alipoanzia, vikwazo
anavyokutana navyo, mafanikio na
matarajio yake kibiashara.
Maziku ni kijana wa Kitanzania aliyezaliwa
mwaka 1990 mkoani Mwanza.
Kitaaluma ni mtaalamu wa masuala ya
kibenki na fedha ambapo alipata Shahada
ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Zanzibar.
Baada ya kuhitimu masomo yake aliajiriwa
katika Benki ya Exim kama ofisa biashara.
Alidumu na kazi hiyo kwa muda mfupi na
kuamua kugeukia biashara ya mazao.
Alipoanzia
Akizungumza na mwandishi wa makala
haya, Maziku anasema alipoona kazi ya
kuajiriwa haina maslahi, aliamua kuanza
biashara ya kusafirisha mazao, hiyo
ilikuwa mwaka 2013.
Anasema alijikita katika biashara hiyo
baada ya kuvutiwa na mjomba yake
aliyekuwa akimiliki mashamba yenye
mazao mbalimbali.
Miongoni mwa mazao ambayo Maziku
alianza nayo na anendelea nayo mpaka sasa
ni korosho, ufuta, mbaazi, choroko, mtama,
alizeti, mashudu ya pamba na pilipili
manga.
Akizungumzia anapoyapata mazao hayo
anasema; “ninachofanya nakusanya mazao
kutoka kwa wafanyabiashara wadogo
wadogo ambao hukusanya mazao kwa
wakulima na katika minada inayofanywa
na vyama vya ushirika mkoani Lindi,
Mtwara, Dodoma, Singida, Shinyanga na
Tanga ambayo hufanyika mara moja kwa
kila wiki.”
Anasema baada ya hapo husafirisha mazao
hayo kutoka mikoani na kwenda
kuyahifadhi kwenye magahala
yanayotumika kuhifadhi mazao.
“Wakati wa kuyafungasha unapofika huwa
nawatumia vibarua na katika vifungashio
vyangu huwa na nembo inayoonyesha jina
la kampuni yangu.
Baada ya hapo sampuli hupelekwa katika
maabara za kupima ubora wa mazao
kimataifa iitwayo SGS,” anasema na
kuongeza:
“Mazao haya huwa nayasafirisha kwenda
nchini Vietnam kwa kutumia meli za
mashirika mbalimbali ikiwamo IPTL,
MAERSK na nyinginezo.”
Anabainisha kuwa huwa hatumii njia za
panya, hufuata hatua zote zinazohitajika
ikiwamo kupata kibali cha Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Kilimo
na Ufugaji, wanasheria pamoja na maofisa
wa usalama wa taifa ambao uhakikisha
hatua zote halali zimefuatwa.
Anasema biashara ya mazao kupeleka nje
ya nchi ina ushindani mkubwa hivyo
inahitaji umakini mkubwa ili kuweza
kujiendeleza, la sivyo unaweza kuishia
njiani kwa kupata hasara.
Anasema anakumbuka alianza na mtaji wa
Sh milioni mbili na sasa anazungumzia
mtaji wa Sh milioni 200.
“Si rahisi kufika nilipofikia, kwa sababu
biashara hii ina ushindani mkubwa.
Ninashindana na matajiri wakubwa wenye
uwezo wa kujipangia bei za mazao hivyo
ingawa nimepiga hatua lakini bado
ninahitaji kupanua biashara yangu zaidi na
zaidi,” anasema.
Anaeleza kuwa mwaka 2013 alipata hasara
ya mamilioni ya fedha baada ya ubora wa
mazao kupimwa na kuonekana upo kwenye
kiwango cha 48 badala ya 51 inayotakiwa,
hivyo alijikuta katika wakati mgumu kwa
kuwa
aliyumba kibaishara kutokana na mtaji
wake kukata.
Maziku anasema ilimlazimu kwenda
kukopa benki ili aendelee kufanya biashara.
“Nilipata hasara kubwa ambayo hadi leo
hii bado ninalipa deni nililokopa benki
ingawa pia fedha kutoka katika biashara
zingine inzozifanya zinaendelea kuifanya
biasahara hii kuendelea kuwapo,”anasema
mfanyabiashara huyo wa kimataifa.
Kila biashara haikosi vikwazo, Maziku
anataja vikwazo wanavyokumbana navyo
kuwa ni mtaji mdogo alionao.
Analia na ukiritimba unaofanywa na benki
mbalimbali ambazo ili kupata mkopo
wanahitaji dhamana kubwa kuliko uwezo
wa mfanyabiashara, jambo
linalokwamishaukuaji wa biashara.
Anataja kikwazo kingine kuwa ni
ukiritimba uliopo kwenye vyama vya
ushirika ambapo hupanga bei zisoendana
na ya soko la dunia.
Anasema hali hiyo inawafanya
wafanyabiashara wengi kushindwa kufikia
malengo.
“Wakati mwingine wafanyabiashara
wenzetu huturudisha nyuma kimaendeleo…
huwa tunawanunulia mazao kwa
makubaliaono ya kulipa baadaye, badala
yake hutoroka na fedha,” anasema.
Pamoja na mambo mengine, anataja
mafanikio aliyoyapata kupitia biashara
hiyo kuwa ni kumiliki kampuni mbili
ambazo ni GEFU Agromart Company
Limited na Lyone investment Company
Limited ambazo
zimeajiri wafanyakazi watano akiwamo
ofisa rasilimali watu, mhasibu, katibu
muhtasi, mwanasheria na meneja
mwendeshaji wa
shughuli za kampuni.
Mafanikio mengine ni kwamba ameweza
kujenga nyumba ya kuishi, kumiliki usafiri
na kupata fursa ya kusafiri kwenda nchi
mbalimbali kuhudhuria makongamano na
maonyesho ya biashara ya mazao, jambo
ambalo limemkutanisha na watu wengi
maarufu hivyo kujikuta akipanua wigo wa
biashara yake kimataifa.
Kwa sasa Maziku anatarajia kufungua
kampuni ya ujenzi ili kuweza kutoa ajira
kwa vijana wengi zaidi wa Kitanzania.
“Pia nina mpango wa kufungua kiwanda
cha kuzalisha juisi, mafuta ya alizeti,
mifuko ya plastiki na maji ya kunywa.
Kiwanda hiki nitakifungua kwa
kushirikiana na wawekezaji kutoka nje ili
nizidi kukuza uchumi wa Tanzania,”
anasema.
Anasema kwa kuwa ana uwezo wa kusaidia
jamii, haoni shida kutoa fedha zake
kuwasaidia wasiojiweza wakiwemo yatima.
“Kidogo nilicho nacho huwa nakitoa na
kwa wenye mahitaji maalumu lakini huwa
sipendi kujitangaza,” anasema
mfanyabiashara huyo.
Maziku anawashauri vijana wenzake kuwa
na uthubutu kama aliokuwa nao yeye,
aliiona fursa akaichangamkia na hadi sasa
amefikia
katika hatua nzuri.
“Vijana tusibweteke, vikwazo ni vingi lakini
hatupaswi kukata tama. Hata
waliofanikiwa kama akina Mo Dewji
hawakuanzia juu. Walipambana na uzuri ni
kwamba wafanyabiasahara wakubwa kama
Mo si wachoyo, huwa wanajitoa kusaidia
wengine kwa kuwapa ushauri wa
kibiasahara
Share:

HAYA NDIO MAZARA YA KUSEMA NA KUAMINI HUWEZI

Mtu anapoamini kwamba hawezi,
anayaambia mawazo yake ya kina
yamsaidie kumfanya ashindwe zaidi
kwenye kila jaribio analofanya. Badala ya
kufanya juhudi kujisaidia ili amudu,
hujipweteka kwa kuamini kwake kwamba
hata kama atafanya kitu gani, kamwe
hatamudu. Siyo rahisi kwa mtu mwenye
mawazo ya aina hii kuweza kufanikiwa
maishani.
Kuna watu ambao kwa sababu ya kukosa
kile ambacho jamii inakiona kuwa ndiyo
ufunguo wa mafanikio, huwa wanaamini
kwamba hawawezi kufanikiwa au kufanya
vizuri maishani kama hao ambao
wanacho. Kwa mfano, kwa kukosa elimu,
ujuzi au utaalamu fulani, watu wengine
hujihesabu kama wanyonge. Huchukulia
kwamba ni wale tu wenye elimu, ujuzi na
utaalamu fulani ndiyo wanaoweza au
wanaotakiwa kufanikiwa.
Bila shaka umeshawahi kusikia au hata
wewe mwenyewe kusema, “Si wamesoma
bwana’ ndiyo wanaojaliwa, sisi ambao
hatuna elimu kazi yetu itakuwa ni
kuwatumikia. Kauli kama hizi zina
chimbuko lake mbali sana, pengine katika
malezi yetu. Wazazi kwalizoea au
wamezoea kuwaambia watoto wao,
“Usiposoma kazi yako itakuwa ni
kuwabebea wenzako mizigo, unafikiri pesa
inaokotwa, nk. Kwa bahati mbaya mtoto
aliyelishwa “sumu” (‘EARLY CHILD
PROGRAMMING’) hii anaposhindwa shule,
huamini kwamba yeye atabaki
kuwatumikia wengine tu.
Tunapoamini kwamba kwa sababu hatuna
elimu ya kutosha na pengine ujuzi au
utaalamu fulani, hatuwezi kufika juu
kwenye mafanikio, tutakuwa tunatafuta
kufulia( ama vifafa vya kiuchumi)


Share:

BILA SHAKA WENGI MNAMFAHAMU MWANAMZIKI HUYU WA KIMAREKANI



Bila shaka watu wengi mnamfahamu
mwanamuziki wa Kimarekani, Katy Perry lakini
inawezekana haufahamu kule alipotoka mpaka
kuwa hapo alipo kwa sasa.
Mwaka 1999, Perry aliamua kuachana na
shule na kujiingiza katika uimbaji. Asili yake
ilikuwa ni muimbaji wa nyimbo za injili,
aliyelelewa kiroho na wazazi wake waliokuwa
walokole kabisa.
Mwaka 2001, Katy Perry akazindua albamu
yake ya kwanza ya nyimbo za injili
aliyorekodia katika Studio ya Red Hill ambayo
haikuwa maarufu wala mafanikio. Baada ya
kuuza kopi 200 tu za albamu yake, studio
aliyoitumia ikaamua kufunga kwani haikuwa
na fedha.
Alichokifanya ni kubadilisha gia, akajitoa
kwenye muziki wa injili na kuingia kwenye
muziki wa kidunia ambapo akaelekea Los
Angeles na kurekodi na studio nyingine
iitwayo Glen Ballard.
Mwaka 2003, akaingia mkataba na Island Def
Jam kwa mkataba ambao baadaye ukafutwa.
Mwaka 2004 akasaini mkataba na Columbia
Records ambao walidhamiria kumfanya kuwa
kiongozi wa bendi yao ya The Matrix. Huko
hakukaa sana kwani napo wakaamua
kuachana naye.
Baada ya kutupwa na lebo tatu, usifikiri
kwamba Perry alikata tamaa, hakukata.
Aliendelea na muziki huku akifanya kazi
mpaka pale aliposaini mkataba na kampuni
ya Capitol Music Group mwaka 2006. Hapo
ndipo alipotoa ngoma kali iliyompa jina ya I
Kissed A Girl ambayo ndiyo iliyomuingiza
katika ulimwengu wa watu maarufu na pia
kumpa mkwanja wa maana.

Kwa nini wewe ukate tamaa kwa changamoto ndogo hizo, jipe moyo na endelea kutengeneza kesho yenye furaha na pesa nyingi.
Share:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES